Welcome | Karibu

Ninatoa mafunzo ya Website Design na Graphic Design kwa njia ya Mtandao na Ana kwa ana. Chagua Unachopenda Kujifunza

Website Design

Mafunzo haya ni kwa ajili ya watu wanaopenda na kutaka kujifunza jinsi ya kutengeneza Website (Tovuti) za kisasa. Utajifunza Jinsi ya kutengeneza website hatua kwa hatua hata kama haufahamu chochote kuhusu Website.

Mafunzo yanatolewa kupitia Channel ya Telegram kwa mfumo wa Videos na katika lugha ya Kiswahili. Hivyo popote ulipo unaweza kujifunza kupitia simu au  kompyuta yako.

Graphic Design

Graphic Design

Kama unahitaji kujua jinsi ya Kutengeneza Logo, Business Cards, Vitambulisho, Matangazo makubwa na madogo basi kozi hii ni kwa ajili yako. Utajifunza Program ya Adobe Photoshop, Microsoft Publisher  na Canva.

Mafunzo yanatolewa kupitia Channel ya Telegram kwa mfumo wa Videos na katika lugha ya Kiswahili. Hivyo popote ulipo unaweza kujifunza kupitia simu au  kompyuta yako.

Waliojiunga na Mafunzo Wanasemaje?

Kozi ya adobe Photoshop imenipa ujuzi mkubwa kuhusu image editing kiujumla, kitu ambacho kimenisaidia katika kufanya project zangu Kwa ufanisi.

Mr. Mwinyimvua

You made it so simple. It’s been great working with you! I have graduated Certificate in Information Technology but I wasn’t taught to design a professional Website. You’re so helpful.

Mr. Mpogolo

Mimi napenda sana ufundishaji wako nimesoma masomo machache, nimeelewa kutengeneza 3D book cover. Be blessed upo clear hata fedha yangu nafeel great nimetoa mahali sahihi.

Mr. Luvanda

Mwalimu Hemedi upo vizuri, unatufanya tujifunze IT bila ya kuingia darasani.

Mr. Rashidi

MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA

01. Ninawezaje kujiunga na mafunzo?

Baada ya kuchagua kozi unayotaka kusoma na kulipia ada, utapatiwa link ya kujiunga na Group la mafunzo, ambalo linapatikana Telegram. Kama hauna Application ya Telegram, Ingia Play Store/App store kisha download ili uweze kujiunga katika mafunzo.

02. Unapatikana wapi? Ofisi zenu ziko wapi?

Mimi ni Mwl. Hemedi, ninapatikana Temeke-Dar es Salaam. Ofisi yangu ipo Temeke, Dar es Salaam. Ila asilimia kubwa huwa nafanya kazi kupitia mtandao wa internet.

03. Mafunzo yanatolewaje?

Mafunzo yanatolewa kupitia kundi la Telegram, Hivyo unaweza Kujiunga Popote ulipo kama una simu yenye uwezo wa internet au Computer. Mafunzo yanatolewa kwa mfumo wa Videos na Katika Lugha ya Kiswahili. Baada ya kuunganishwa katika Kundi la Mafunzo, unaweza kudownload videos na kuangalia kupitia simu yako au Kompyuta.

04. Nitajuaje kama kweli unatoa mafunzo?

Kama una mashaka/wasiwasi na hauna uhakika juu ya mafunzo tunayotoa unaweza kuwasailiana nami kupitia Whatsapp 0672999266 Kisha utatumiwa Video ya mafunzo ya mfano (Sample Video) bila kulipia chochote.

05. Ninaweza kujiunga na program moja tu?

Ndio, sio lazima usome mafunzo yote tunayotoa. Unaweza kuchagua program ya kusoma ambayo una uhitaji nayo. Baada ya kuchagua program husika utalipia ada yake na baada ya kuunganishwa na mafunzo utaanza kusoma muda huohuo.

06. Mafunzo yanachukua muda gani?

Mafunzo yote yamerekodiwa katika mfumo wa videos, Hivyo baada ya kujiunga na mafunzo husika unaweza kuanza kudownload na kuangalia video za mafunzo. Hivyo muda wa kukamilisha kusoma mafunzo husika kutategemea na muda unaoutumia kujifunza na uharaka wa kuelewa mafunzo. Kwa wastani kumaliza mafunzo kunaweza kukachukua wiki 1 hadi 2.

Jiunge na Mafunzo ya Bure Telegram

Scroll to Top