KWA NINI NI LAZIMA UJIFUNZE MICROSOFT EXCEL, SABABU 5 ZA MSINGI

MAFUNZO YA MICROSOFT EXCEL FOR BUSINESS

Microsoft Excel ni Program ya kimahesabu inayotumika kuhifadhi data katika muundo wa nambari, maneno, grafu na chati. Microsoft Excel inatumika katika makampuni biashara na katika taasisi mbalimbali. Pia watu binafsi hutumia program hii kwa matumizi mbambali. Kuna sababu tano za msingi za wewe kujifunza  Microsoft Excel.

1.Kuongeza ufanisi katika kazi.

Program ya microsoft excel inakusaidia kuongeza ufanisi katika kazi unazofanya kutokana na uwezo wake wa kurahisisha kazi na kuokoa muda. Mfano kama ulitakiwa kutengeneza ripoti 100 kwa njia ya mkono ungeweza  kutumia hata siku nzima kuandaa tu, lakini kupitia Microsoft excel unaweza kukamilisha kazi hiyo ndani ya saa 1 au masaa mawili tu.

2.Kutunza taarifa binafsi.

Unaweza kutumia program ya Microsoft Excel  kutunza taarifa zako binafsi kama vile orodha ya vitu, bajeti yako binafsi au kufanyia mahesabu muhimu ya manunuzi / matumizi unayoyafanya.

3.Kufanya mahesabu ya kibiashara.

Program ya Microsoft excel ina umuhimu mkubwa sana katika biashara. Uwezo wake wa kufanya mahesabu kiutomatiki ndio unaoipa umuhimu huo. Microsoft Excel  katika biashara inatumika kutunzia taarifa za mauzo, taarifa za wateja  pamoja na kufanya mahesabu na michanganuo  ya mauzo pamoja na kuandaa ripoti.

 

4.Kujiongezea sifa ya kuajiriwa.

Dunia imebadilika sana na teknolojia ndio kila kitu katika maisha yetu ya sasa. Kutokana na umuhimu mkubwa wa program hii ya Microsoft Excel makampuni na taasisi nyingi huwa wanahitaji watu wenye uwezo wa kutumia computer ikiwemo na program hii ya Microsoft Excel. Hivyo kujifunza Microsoft Excel ni Kujiongezea sifa muhimu inayohitajika na waajiri wengi katika kipindi hiki.

 

5.Kutengeneza Kalenda.

Kalenda ni nyenzo muhimu ya kudhibiti muda kwa kupangilia muda na matukio au kazi tunazojipangia kutekeleza katika muda husika. Kupitia program ya Microsoft Excel unaweza kuandaa kalenda binafsi, kalenda ya ofisi au Kalenda ya mwaka ikionyesha miezi yote 12 na matukio muhimu katika mwaka husika.

Kalenda-excel

 

Unawezaje Kujifunza Microsoft Excel

Hakuna sababu ya kusema sina muda wa kujifunza au hakuna wanapofundisha. Siku hizi unaweza kujifunza kila kitu bila kuondoka nyumbani kwako. Mtandao umefungua vikwazo vyote vya kujifunza na hivyo hautaji tena kusafiri umbali mrefu kusoma Microsoft Excel. Unaweza kujifunza Microsoft Excel kupitia simu yako au kompyuta yao ukiwa nyumbani kupitia makala zilizopo mtandaoni au Videos kupitia YouTube. Kama bado hujajiunga na Channel yangu Bofya hapa Ujiunge ili Kujifunza Microsoft Excel bure.

 

Karibu katika Mafunzo ya Microsoft Excel for Business, kozi ambayo ni kozi ambayo imelenga kukupa maarifa sahihi ya kudhibiti taarifa na mahesabu ya biashara yako kwa ufanisi mkubwa. Pia utajifunza mbinu za masoko. BONYEZA HAPA KUJIUNGA

One Comment

Leave a Comment

Scroll to Top